Majanga ya Pasaka!!! ASKARI POLISI AVUNJWA MGUU SHINYANGA, WENGINE WATANO WAJERUHIWAGari lenye namba za usajili T684 AYJ likiendeshwa na Emmanuel Charles Kazungu(43) mkazi wa Kitangiri limeacha njia katika eneo la kanisa katoliki Shinyanga mjini barabara ya Uhuru na kuwaparamia watembea kwa miguu akiwemo askari polisi H.4515 PC Geofrey ambaye amevunjika mguu wa kushoto.


Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo /siku ya mkesha wa pasaka majira ya saa nane usiku,ambapo mbali na kumjeruhi askari huyo pia watu wengini watano wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyang ACP Dismas Kisusi Kamanda Kisusi amewataja majeruhi wengine kuwa ni Majid Abdul(25)mkazi wa Kizumbi,Mashaka Juma (25) mkazi wa Katunda,Joseph Shija(22) mkazi wa viwanja vya Mwadui,Tendea Lutema(25) mkazi wa Old Shinyanga na Idd Magembe(30) mkazi wa Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva na tayari jeshi la polisi linamshikilia dereva huyo kwa hatua zaidi za kisheria.
Gari iliyosababisha ajali ikiwa eneo la tukio


Picha kwa hisani ya  Ommy Fashion

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post