Majanga Shinyanga!! JAMAA AJICHOMA MISUMARI KICHWANI KISHA KUJINYONGA KWA KAMBA CHUMBANI KWAKE

NB-Picha haihusiani na habari hapa chini

 
Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina la Godwin Paul Kalulu(43) fundi seremala mkazi wa Majengo ya zamani mjini Shinyanga amekutwa amefariki kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ndani ya chumba chake huku kichwa chake kikiwa kimechomwa misumari miwili.


Kwa mujibu wa taarifa ya kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Dismas Kisusi tukio hilo limetokea juzi saa 12 asubuhi katika mtaa wa Majengo ya Zamani mjini Shinyanga ambapo Kalulu alikutwa amejinyonga ndani ya chumba chake.

Kamanda Kisusi alisema Godwin Paul Kalulu alikutwa amejinyonga kwa kamba aliyokuwa ameifunga katika kenchi ya chumba chake.

Aliongeza kuwa mwili wa marehemu ulikutwa na misumari miwili katika kichwa chake.

Kisusi alisema kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa ndugu wa marehemu,walisema siku tatu kabla ya kifo chake,marehemu alionekana kutokuwa sawa kiakili na walimpeleka rufaa ya mkoa wa Shinyanga kupata matibabu na kwa uchunguzi wa daktari marehemu hakukutwa na ugonjwa wowote.

Alisema ndugu wa marehemu waliendelea kueleza kuwa marehemu alikuwa akitamka maneno kwamba kuna watu wanamfuatilia wakiwa na bunduki na wanataka kumuua.

Kamanda Kisusi alisema jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linaendelea kufanya uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post