HAPPY BIRTH DAY TO YOU DJ HUNTER,MDAU MKUBWA WA MALUNDE1 BLOG
Anaitwa Athanas Phabian a.k.a Dj hunter ni mtangazaji na mwandishi wa habari kwa miaka kadhaa toka alipohitimu chuo cha uandishi cha jijini Dar es salaam mwaka 2009.
 Mpaka sasa ametimiza ndoto yake ya kuwa Dj wa kimataifa kwenye kituo kimoja nchini Ujeruman radio Leinehertz.
Tofauti na kazi ya  Udj jamaa anapiga kazi mgodini.
Alizaliwa tarehe kama ya leo Machi 13  huko Singida Miaka Kibao iliyopita.
Ni miongoni mwa Madj wasiopenda sifa ila anaonekana kulingana na ubunifu wake na bidii anazofanya radio alizopita ni Chuchu fm Zanzibar 2010 ,Radio Faraja Fm ya Shinyanga mwaka 2012~2015.
Hivi sasa ni mshirika wa radio ya kimataifa ya nchini Ujerumani akifanya kipindi cha Bongo 106.5 akiwa na Veronica Natalis.
Dj Hunter ni miongoni mwa wadau muhimu wa  Malunde blog,ndiyo miongoni mwa watu waliochangia blog hii kujulikana kimataifa na pia ndiyo anajua siri ya blog hii kuitwa Malunde1 blog
Happy Birthday brother Dj Hunter!!!
Hizi hapa ni baadhi tu ya picha zake
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post