ASKARI POLISI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI SIKU YAKE YA KWANZA KAZINI



Polisi mmoja wa kike nchini Marekani amepigwa risasi na kuuawa katika siku yake ya kwanza kazini.

Askari huyo bi Ashley Guindon alikula kiapo mapema siku hiyo hiyo kisha akaelekezwa na wakubwa wake kwenda nyumbani kwa mama mmoja kutatua mzozo wa kinyumbani katika kitongoji Washington, DC.

Bi Ashley akiandamana na wenzake wawili walikwenda Woodbridge, Virginia, kilomita 32 kusini mwa Washington lakini walipofika huko walifyatuliwa risasi na kwa bahati mbaya Ashley hakubahatika.



Wenzake wawili pia walijeruhiwa vibaya na wamelazwa hospitalini.



Mshukiwa wa mauaji hayo ni mlengaji shabaha katika jeshi la Marekani aliwazidi maarifa maafisa hao wachanga.

Mwanjeshi huyo alikamatwa baadaye na vitengo maalum vya polisi.

Mwanjeshi huyo alikuwa amempiga risasi na kumuua mkewe papo hapo kabla ya Ashley na wenzake kutokea.

Hakukuwa na mtoto nyumbani wakati wa ufyatulianaji huo wa risasi.

Afisa mkuu wa kituo " Tunasikitika kuwatangazia kifo cha afisa wa polisi wa kituo cha Prince William County bi,Ashley Guindon, aliaga dunia kufuatia ufyatulianaji risasi katika mtaa wa Lashmere Ct akiwa kazini.



Mapema siku hiyo hiyo kituo hicho kilikuwa kimetoa picha ya afande huyo kwenye mtandao wa Twitter ikimkaribisha kwa huduma kwa wote.

''Tunafurahi kuwakaribisha afande Ashley Guindon na mwenzake kwa huduma kwa wote''
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post