ANGALIA PICHA 24 -MKUU MPYA WA MKOA WA SHINYANGA ANNE KILANGO MALECELA AKITAMBULISHWA KWENYE MKUTANO WA VIONGOZI WA MKOA WA SHINYANGA


Leo Jumatatu ya tarehe 21.03.2016 mkuu mpya wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela amekabidhiwa ofisi ya mkoa wa Shinyanga na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Nassoro Rufunga.Kilango amechukua nafasi ya Rufunga baada ya kuteuliwa na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli hivi karibuni.


Baada ya kukabidhiwa ofisi hiyo,Malecela alitambulishwa kwa viongozi mbalimbali wa serikali ngazi ya wilaya na mkoa,taasisi za kidini,waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani humo.Pichani ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga wakati wa zoezi la utambulisho-Picha zote na Kadama Malunde na Magdalena Nkulu-Malunde1 blog


Aliyesimama ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi akiwatambulisha wageni waalikwa katika mkutano huo wa kumtambulisha mkuu mpya wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela(kushoto),kulia ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Kanali mstaafu Tajiri Maulid
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiwaaga viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakati akimtambulisha Anne Kilango Malecela kuwa ndiyo mkuu wa mkoa wa ShinyangaRufunga alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha watumishi wa umma wazembe kuchapa kazi na kuacha majaribio katika kazi kwani serikali ya awamu ya tano ni ya aina yake ni imedhamiria kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi.Pichani ni wenyeviti wa halmashauri za wilaya za Mkoa wa Shinyanga Rufunga aliwataka watendaji kushirikiana na mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.Kulia ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Hawa Ng'humbi akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Vita KawawaRufunga aliyeanza kutumikia mkoa wa Shinyanga tangu Oktoba 04,2011 mpaka mwezi Machi Mwaka huu aliwapongeza waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya kuutangaza mkoa wa Shinyanga na kuihabarisha jamii kuhusu mambo mbali yanayoendelea mkoani humo-Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifuatilia kwa umakini hotuba fupi ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiwaaga viongozi na wananchi wa Shinyanga
Mkutano wa utambulisho unaendelea...pichani mstari wa mbele ni wenyeviti wa halmashauri za wilaya katika mkoa wa ShinyangaAliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akimkaribisha mkuu mpya wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela wakati wa mkutano huo wa utambulishoViongozi wa halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbiniMkuu mpya wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela akizungumza wakati wa mkutano wa kutambulishwa kwake kwa viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga.Kilango aliyejinadi kuwa mzoefu katika kazi za serikali na kuwatumikia wananchi akitolea mfano wa miaka 15 ya ubunge,aliwataka watendaji katika serikali kujitahidi kufanya kazi usiku na mchana kwani wananchi walio wengi ni maskini na wanategemea viongozi wachapakazi ili kuwaondoa katika hali hiyo.Kilango alisema wananchi wanataka viongozi wachapa kazi ili kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo upungufu wa madawati katika hivyo akawaomba ushirikiano ili kuwaletea maendeleo wananchi-Kulia ni askofu wa kanisa katoliki Jimbo la Shinyanga mhashamu Liberatus Sangu akiwa na Askofu mkuu wa kanisa la AICT dayosisi ya Shinyanga Dkt John Kanoni Nkola wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbiniKushoto ni Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akiwa na wajumbe wengine wa mkutano huoMstari wa kwanza mbele-Viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Shinyanga wakiwa ukimbiniMkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela alitumia fursa hiyo kuwaomba watendaji wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya na wakurugenzi kushirikiana naye katika kumaliza tatizo la upungufu wa madawati katika shule,kupiga vita mauaji ya vikongwe na albino na kuongeza kuwa mkoa huo hauna tatizo kubwa la wafanya kazi hewaPicha ya pamoja,aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Nassoro Rufunga(kushoto),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi na wakuu wa wilaya za mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kishapu,Shinyanga na KahamaPicha ya pamoja,aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Nassoro Rufunga(kushoto),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa ShinyangaPicha ya pamoja,aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Nassoro Rufunga(kushoto),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi na viongozi wa vyama vya siasaPicha ya pamoja,aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Nassoro Rufunga(kushoto),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi na wenyeviti wa halmashauri 6 za wilaya mkoa wa ShinyangaPicha ya pamoja,aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Nassoro Rufunga(kushoto),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi na viongozi wa madhehebu ya diniPicha ya pamoja,aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Nassoro Rufunga(kushoto),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi na wakurugenzi wa halmashauri 6 za wilaya mkoa wa ShinyangaPicha ya pamoja,aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Nassoro Rufunga(kushoto),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi na makatibu tawala wa wilaya tatu za mkoa wa ShinyangaPicha ya pamoja,aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Nassoro Rufunga(kushoto),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi na sekretariati ya mkoa wa ShinyangaPicha ya pamoja,aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Nassoro Rufunga(kushoto),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi na baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa ShinyangaPicha ya pamoja,aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Nassoro Rufunga(kushoto),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi na baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde na Magdalena Nkulu-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527