Angalia Picha!! HATIMAYE DR SLAA AFUNGA NDOA NA JOSEPHINE MUSHUMBUSI



Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi.


Wawili hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa moja, lakini habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.


Ndoa hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu za Dr Slaa ambaye mwaka 2010 aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani akidai bado anamtambua Josephine kuwa ni mke wake wake halali.


Mume huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama impatie haki yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa.




Misukosuko ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa mke wake, Rose Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50.


Dr Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini lakini wakashindwa kutokana na mapingamizi hayo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527