Picha 45!! TGNP MTANDAO YAENDESHA WARSHA YA SIKU MBILI SHINYANGA KUHUSU UCHAGUZI MKUU 2015 TANZANIA


Hpa ni katika ukumbi wa mikutano wa Katemi Hotel katika eneo la Ngokolo Mitumbani mjini Shinyanga ambako kumefanyika
warsha ya siku mbili ya kufanya tathmini ya mpango mkakati wa TGNP Mtandao wa kuwajengea uwezo wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu mwaka 2015 iliyofanyika mjini Shinyanga.Washiriki wa warsha hiyo wametoka katika mikoa ya Shinyanga,Mara na Simiyu.Washiriki wametumia fursa hiyo kujadili changamoto walizokabiliana nazo wanawake,vijana na watu wenye ulemavu katika uchaguzi uliopita na kujadili mikakati mbalimbali ya kufanikisha malengo yao katika chaguzi zijazo.


Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde amehudhuria warsha hiyo,ametuletea picha zifuatazo.....Siku ya Kwanza-Februari 04,2016-Mwezeshaji wa warsha hiyo Dinah Nkya kutoka TGNP Mtandao akizngumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ambapo alisema lengo kuu la warsha mrejesho hiyo ni kupima utekelezaji wa mpango kazi waliojiwekea washiriki baada ya mafunzo ya awali yaliyoanza mwaka 2014 kwa kuangalia namna walivyotumia nafasi zao,ushawishi wao katika kuelimisha jamii kuhusu ushiriki wa wanawake,vijana na walemavu katika mchakato wa uchaguzi na uongozi wa siasa.Baadhi ya Washiriki kutoka mkoani Mara wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbiniBaadhi ya washiriki kutoka wilaya ya Kahama wakiwa ukumbiniBaadhi ya washiriki kutoka manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbiniWashiriki wakiwa ukumbini
Washiriki wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini

Mwezeshaji kutoka TGNP Mtandao Rebeca Mjema Kisena akizungumza katika warsha hiyo ambapo alisema katika uchaguzi mkuu 2015 wa madiwani,wabunge na rais kumekuwa na ongezeko la wanawake,vijana na watu wenye ulemavu katika nafasi za ubunge na udiwani kutokana na mradi wa uchaguzi wa TGNP mwaka 2014/2016 wa kuhamasisha makundi hayo kushiriki katika chaguzi mbalimbali

Washiriki katika warsha hiyo wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbiniMwandishi wa habari kutoka Radio Faraja Moshi Ndugulile akiwa ukumbiniKushoto ni Mwezeshaji msaidizi kutoka TGNP Mtandao Ernest Mpalile akijaza dodoso wakati wa mahojiano na mmoja wa washiriki wa warsha hiyo ,Veronica Natalis kuhusu namna alivyoshiriki katika kutekeleza mradi wa uchaguziKushoto ni Mwezeshaji wa warsha hiyo Dinah Nkya kutoka TGNP Mtandao akifanya mahojiano na mshiriki wa warsha hiyo Bonny Matto kutoka Tarime mkoani Mara
Siku ya Pili ya warsha Februari 05,2016-Wawezeshaji katika warsha hiyo kutoka TGNP wakiteta jambo ukumbiniWashiriki wa warsha hiyo wakifanya kazi za makundiMjadala unaendeleaWaandishi wa habari wakiwa ukumbiniKushoto ni Mwezeshaji msaidizi kutoka TGNP Mtandao Ernest MpalileWashiriki wakiimba wimbo kuhusu usawa wa kijinsiaTunaimba wimbo......
Washiriki wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Marco Mkanjiwa,ambaye ni mwenyekiti wa Shirikisho la watu wenye ulemavu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga akizungumza ukumbiniMraghabishi kutoka shirika la Sheria na Haki za Binadamu Tarime mkoani Mara ,Bonny Matto akiwa ukumbini

Mwezeshaji kutoka TGNP Mtandao Rebeca Mjema Kisena akizungumza ukumbiniTunafuatilia kinachoendelea ......Warsha inaendeleaBwana Iddy Mpyalimi akichangia mada ukumbini

Mwandishi wa habari Moshi Ndugulile akieleza namna vyombo vya habari vilivyotumika kuhamasisha wanawake,vijana na walemavu kushiriki katika uchaguzi mkuu mwaka 2015

Mwandishi wa habari Masanja akizungumza ukumbini

Mkurugenzi wa Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga,bwana Kadama Malunde,akiwa ukumbini

Kulia ni bwana Marco Maduhu mwandishi wa habari gazeti la Nipashe akiwa na bwana Frank Mshana mwandishi wa habari ITV na Radio One

Washiriki wakiwa katika kazi ya kikundi

Washiriki wakiwa katika kazi ya kikundi
Kazi za makundi zinaendelea


Washiriki wakiwa katika kazi ya kikundiWawezeshaji wakiteta jambo ukumbini,kulia ni Dinah Nkya akiwa na Rebeca MjemaWashiriki wakiimba ukumbiniWawezeshaji na washiriki wa warsha hiyo wakiimba na kucheza ukumbiniMshiriki wa warsha hiyo Marry kutoka manispaa ya Shinyanga akiwasilisha kazi ya kundi lakeMratibu wa warsha hiyo bi Janeth Mawinza akizungumza ukumbiniBwana Masanja kutoka mkoani Simiyu akiwasilisha kazi ya kundi lake


Bwana Bonny Matto kutoka mkoani Mara akiwasilisha kazi ya kundi lakeKushoto ni mwezeshaji msaidizi kutoka TGNP Elieth Samwel Eliyuko,akifuatiwa na mwezeshaji msaidizi Ernest Mpalile na mratibu wa warsha hiyo Janeth Mawinza
Picha ya pamoja baada ya warsha kumalizika Februari 05,2016Picha ya pamoja washiriki wotePicha ya pamoja- Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post