Picha 26 !! KWILASA ASHINDA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA,NDIYO MRITHI WA MGEJA WA CHADEMA,ABARIKIWA NA MVUA

 

Msimamizi mkuu wa uchaguzi wa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Shinyanga leo ndugu Abdalah Bulembo ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM taifa akizungumza katika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga leo baada ya uchaguzi wa awamu ya kwanza ambapo wagombea walipata kura ambazo hazifiki nusu ya wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga waliopiga kura.Bulembo alitangaza uchaguzi urudiwe,Wagombea wa kiti hicho walikuwa watatu ambao ni Hassan Mwendapole aliyepata kura 21,Mabala Mlolwa kura 395 na Erasto Kwilasa kura 384 katika uchaguzi wa awamu ya kwanza-Fuatilia hapa chini Matukio yaliyojiri-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga
Masanduku ya kupigia kura yakiwa tayari kwa ajili ya uchaguzi wa awamu ya pili leo,ambapo msimamizi wa uchaguzi huo Abdalah Bulembo alisema mgombea aliyepata kura chache zaidi katika uchaguzi wa awamu ya kwanza hatahusika katika uchaguzi wa awamu ya pili badala yake wagombea watakuwa wawili tu ambao ni Kwilasa na Mlolwa
Wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga wakiwa katika foleni ya kupigia kura
Tunasubiri kupiga kura...
Wakati zoezi la kupiga kura linaendelea Mvua ilianza kunyesha...zoezi likasitishwa kwa muda....
Wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga wakisubiri mvua ikatike ili waendelee na zoezi la kupiga kura
Maboksi ya kupigia kura yakaondolewa kwenye mvua na kulindwa 
Meza kuu ikawa haikaliki kutokana na mvua kuendelea kunyesha
Wapiga kura wengine wakaamua kukimbilia kwenye jukwaa kuu la uwanja wa CCM Kambarage kwa ajili ya kujikinga na mvua
Ilikuwa mvua ya upepo lakini wenye roho ngumu wakavumilia kwenye mabanda yaliyokuwa uwanjani hapo huku waliokuwa kwenye jukwaa la uwanja nao wakilowana pamoja na kwamba waliamini kuwa watajikinga na mvua
Hata kabla ya matokeo kutangazwa tayari Wanaccm walikuwa wameanza kusherehekea,hatukujua kama ni muziki mnene wa nyimbo za CCM ama pengine walikuwa wameshajua nani kashinda nafasi hiyo ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga
Tunasubiri matokeo yatangazwe....
Kada wa CCM akicheza kabla ya matokeo kutangazwa
Makada wa CCM wakiteta jambo wakati wanasubiri matokeo yatangazwe
Wanacheza na kushangilia kabla ya matokeo kutangazwa
Muda Ukawadia...Msimamizi wa uchaguzi Abdalah Bulembo akitangaza matokeo ya uchaguzi huo,ambapo alisema jumla ya wajumbe wa kamati kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga waliopiga kura katika uchaguzi wa pili ni 814,kura zilizoharibika ni tano,kura halali zilizopigwa ni 809,ambapo alimtangaza Kwilasa kushinda kwa kura 427 huku Mabala akiambulia kura 382.
Kwilasa anachukua nafasi ya Khamis Mgeja aliyetimukia Chadema mwezi Sepetemba 2015 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu kwa madai kuwa CCM imekosa mwelekeo.Kwilasa ataongoza chama hicho kwa muda wa mwaka mmoja na nusu kabla ya kufanyika uchaguzi mwingine nchi nzima kutafuta wenyeviti wa mikoa.
Kushoto ni ndugu Mabala Mlolwa ambaye akizungumza baada ya matokeo kutangazwa,ambapo alisema amekubali matokeo na kuahidi kumpa ushirikiano mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Shinyanga
Kulia ni msimamizi wa uchaguzi Abdalah Bulembo akimkaribisha mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Erasto Kwilasa(kushoto),Bulembo alimpongeza Kwilasa kwa ushindi huo na kumtaka kufanya kazi kwani sasa ni Hapa Kazi tu
Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akiwashukuru wapiga kura kwa kumchagua kuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,ambapo aliahidi kuondoa makundi ndani ya chama hicho
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akizungumza na wanachama wa CCM katika uwanja wa CCM Kambarage huku msimamizi wa uchaguzi huo Abdalah Bulembo akisikiliza kwa umakini maneno ya Kwilasa
Makada wa CCM wakiwa eneo la tukio
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akizungumza baada ya ushindi
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akisisitiza jambo 
Hapakuwa na muda tena wa kucheza wala kushangilia ushindi..Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa anaondoka uwanjani baada ya kutoa hotuba fupi 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akiondoka uwanjani
Makada wa CCM wakisukumagari la mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa. 
Kwilasa anayetokea katika wilaya ya Shinyanga alikuwa anachuana na Mabala Mlolwa kutoka wilaya ya Kahama na Hassan Mwendapole kutoka wilaya ya Shinyanga,ambapo Mabala alipata kura 382 katika uchaguzi wa awamu ya pili baada ya kura za uchaguzi wa awamu ya kwanza mshindi kutovuka nusu ya kura zote.
Katika uchaguzi wa awamu ya kwanza Kwilasa alipata kura 384,Mabala Mlolwa kura 395 huku Hassan Mwendapole akipata kura 21 hali iliyopelekea Msimamizi wa Uchaguzi huo Abdalah Bulembo ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM taifa kutangaza uchaguzi urudiwe kwa wagombea wawili ambao ni Erasto Kwilasa na Mabala Mlowa.
Uchaguzi wa awamu ya pili ulimalizika kwa kumfanya Kwilasa kumbwaga chini Mabala aliyekuwa ameongoza katika uchaguzi wa awamu ya kwanza.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527