NYUMBA ZA WANANCHI ZANZIBAR ZIKO HATARINI KUCHUKULIWA NA BAHARI



Nyumba za wananchi za Kilimani Zanzibar ziko hatarini kudidimia na kuchukuliwa na bahari kutokana na mabadiliko ya tabia nchi huku serikali ya muungano ikiahidi kuchukua hatua za maksudi za kuzinusuru na uharibifu huo. 



Msimamo huo wa serikali umetolewa na naibu waziri wa muungano na mazingira wa serikali ya muungano mhe Luhanga Mpina baada ya kutembelea maeneo yaliyukubwa na uharibifu huo katika eneo la Kilimani Zanzibar ambapo alishuhudia maji ya bahari yanavyotafuta ardhi na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira ambapo naibu waziri amesema fedha zipo na kutaka upandaji na uwekaji wa matuta unaanza mara moja.

Mapema mkurugenzi wa mazingira wa Zanzibar Juma Bakari Alawai amesema mabadiliko ya tabia nchi yahatarisha eneo hilo na endapo hatua za haraka hazita chukuliwa eneo hilo lote litageuka bahari na kuhatarisha maisha ya wananchi na maendeleo ya nchi.

Naibu waziri Mpina anakuwa waziri wa kwanza anayeshugulikia masuala ya muungnao kufika Zanzibar na kungalia kero na matatizo ya wananchi na kutekeleza hatua hizo kwa vitendo na kutoa ahadi za uhakika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527