MFANYAKAZI WA TANESCO APEWA KICHAPO NA WANANCHI HUKO MOROGORO,KISA NGUZO ZA UMEME



Wananchi wa kijiji cha Lumuma wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wameandamana kwa kufunga barabara na kumpiga mfanyakazi wa shirika la ugavi wa umeme Tanesco wakilalamikia shirika hilo kupitisha nguzo za umeme kwenye mashamba yao kupeleka nishati hiyo katika vijiji jirani bila wao kupatiwa huduma hiyo. 
 
 
Wakizungumza kijijini hapo wananchi hao wamesema wameamua kuandamana na kufunga barabara kufuataia shirika la umeme Tanesco kushindwa kusambaza huduma hiyo katika kijiji hicho na badala yake kupitisha nguzo katika maeneo yao kupeleka huduma katika vijiji vya jirani ambapo wamesema hawapotayari kuruhusu mradi huo kuendelea hadi watakapohakikishiwa kuunganishiwa nishati hiyo. 
 

Nao viongogozi wa kata na kijiji cha Lumuma wamesema wanaunga mkono wananchi kwani wamesema inaonekana zoezi hilo limegubikwa na hujuma huku wameomba serikali na uongozi wa Tanesco kuona uwezekano wa kuanza kusambaza umeme katika kijiji cha Lumuma na badaye kumalizia katika vijiji vilivyoko katika kata hiyo.
 

Akiongea na ITV kwa njia ya simu meneja Tanesco mkoa wa Morogpro Mhandisi John Bandiye amesema anatambua kuwepo mradi wa umeme katika kata ya Lumemo lakini hafahamu kama wananchi wa kijiji hicho wanalalamika na kwamba atafuatilia ili kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo. 
 
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527