KITUO CHA KUZALISHA UMEME TANESCO GONGO LA MBOTO CHAUNGUA MOTO



Kituo cha kuzalishia umeme chenye uwezo wa 15 mva cha shirika la umeme nchini Tanesco cha Gongolamboto jijini Dar es Salaam
mtambo wake wa kusambazia umeme umeungua moto kufuatia hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye kifaa cha socket break kilichoanza kufanya kazi tangu mwaka 1952 kushindwa kufanya kazi na kusababisha vifaa vingine kuharibika kwa kuwaka moto.
 
 
Akizungumza katika eneo hilo meneja wa Tanesco mkoa wa Ilala injinia Athanasius Nangali amesema moto huo ulizuka katika jengo la chumba cha mtambo huo maarufu kama control room majira ya usiku na kusababisha maeneo kadhaa yanayopata huduma hiyo kutoka kwenye kituo hicho kukosa umeme licha ya kuwahi kuuzima moto huo.

Aidha, injinia Nangali pamoja na kutojua hasara ya uharibifu wa vifaa iliyopatikana hadi sasa licha ya kuwaomba radhi wateja wa shirika hilo kwa usumbufu walioupata kwa kukosa umeme amesema kituo kipya kilichojengwa pembeni ya kituo hicho kina uwezo zaidi ya mara tatu ya kilichopo jambo litakalomaliza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya uhakika ya umeme kwa wananchi wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527