Duh!! MBUNGE AVUNJA REKODI YA SHINDANO LA KUBUSU,BUSU LAKE LANASA KWA MKEWE MUDA MREFU HAIJAWAHI KUTOKEA


Mbunge Joseph Chinotimba Zimbabwe


Bwana Chinotimba na mkewe Vimbai

Mbunge mmoja nchini Zimbabwe Joseph Chinotimba ameingia katika kumbukumbu za Afrika baada ya kumbusu mke wake Vimbai kwa muda mrefu zaidi kuwahi kunakiliwa barani Afrika.

Mbunge huyo na mkewe walizoa tuzo hilo baada ya kupigana busu kwa dakika 10 na sekunde 17.

Rekodi hiyo iliwekwa katika hafla moja iliyopigiwa upatu na kunadiwa kuwa ''Mashindano ya busu refu zaidi kuwahi barani Afrika''

Hafla hiyo ilipangwa na kuandaliwa kwa ushirikiano na waandalizi wa Daftari la rekodi barani Afrika.

Hafla hiyo iliandaliwa katika mji mkuu wa Harare kama sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao iliyoadhimishwa jumapili.

Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527