Angalia Picha!! KIJANA AFARIKI KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA SHINYANGA,TAHARUKI YAIBUKA MSIBANI,ALIANZA KWA KUPANDISHA MAJINI


Wananchi wa kata ya Kambarage wakiaga mwili wa Emilian Kulwa anayedaiwa kufariki katika mazingira ya kutatanisha-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog



Awali wananchi wakiwa katika eneo la tukio wakimsikiliza diwani wa kata hiyo Hassan Mwendapole

Diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akiwasihi wananchi wasifanye vurugu msibani

Mwili wa marehemu ukiletwa kutoka hospitalini


Katika hali isiyo ya kawaida wananchi wa mtaa na kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga wamezua kizaazaa msibani wakishinikiza kuaga mwili wa marehemu Emiliani Kulwa (26) aliyefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha baada ya kuanza kupandisha majini na kutamka maneno yasiyoeleweka.


Taharuki hiyo ilitokea jana jioni baada ya mwili wa marehemu kushindwa kuwasilishwa msibani  kwa ajili ya wananchi kuuaga kwa madai kuwa umeharibika vibaya na hauwezi kuagwa.

Mwili wa marehemu ulitakiwa uwasilishwe msibani hapo majira ya saa kumi jioni kwa ajiri ya wananzengo kuuaga na kisha urudishwe mochwari kuandaliwa kwa safari ya kupelekwa kwao na marehemu Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.

Wakati wananchi hao wakisubiri mwili wa marehemu kuletwa kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ghafla wanazengo ambao walitumwa kuufuata walirudi huku gari likiwa tupu, wakati jamii ikitangaziwa ikaupokee lakini cha ajabu wakakuta mwili huo haupo ndipo vurugu, miruzi, yowe zilipoanza kutawala msibani hapo.

Baada ya hali kuendelea kuwa mbaya diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole alifika eneo la tukio na kutuliza hasira za wananzego na  na hatimaye mwili ukaletwa msibani hapo majira ya saa 12 jioni hali iliyofanya wanazengo kuushangilia na hatimaye vurugu kuisha.


 Mdau wa Malunde1 blog Agnes Lema  kutoka Kambarage aliyekuwa eneo la tukio ameisimulia blog hii kuhusu tukio hili….

“Kuna huyo kijana aliugua kichwa akapelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga inadaiwa kuwa hakuwa na  damu ..akiwa hospitalini akaongezewa ..kisha kuna maombi yalifanyika mara akapandisha majini,jini likawa linasema limetumwa ila halijataja limetumwa na nani….

Ikabidi kijana  atolewe hospitali arudishwe nyumbani…basi ikawa mara maombi mara waganga wa kienyeji sasa akiwa home kwao hapa jirani, ndiyo mauzauza yakawepo sasa hasa nyakati za usiku….

Mara mgonjwa awataje watu wanaojulikana hapa hapa mtaani kwamba “Niacheni mnanichukua mie wanini sasa wakati sina hata kitu..Basi mambo mengi yakawa yanatokeo ndani ,wakifanya maomba jini linapanda likaongea mengi sikuwepo ila kwa maelezo kuwa ni lazima afe..

Kutokana na mauza uza hayo ikabidi ndugu waite ambaye naye aliomba dua akasema “Huyu Jini mkubwa mpaka aje Mtu mwenye Jini mkubwa zaidi ya huyu”,Anasimulia Agnes Lema.

“Asubuhi yake ndiyo mgonjwa alifariki dunia kwani alikuwa hoi hainuki wala nini ..pia kuna taarifa kuwa usiku huo aliinuka na kufungua mlango kisha kutoka nje mpaka kwenye chumba ambacho hakijaisha kujengwa akawa anaita majina flani na kuwaambia “Mnanipeleka wapi basi kateni fensi ili nipite mbona sioni ninapoenda… na mnaning’ang’ania nimewakosea nini”….

Mambo mengi alizungumza , kakaake akamwambia kama wamegoma kukata fensi turudi, akarudi kitandani akakaa na kuongea na ndugu yake mambo mengi pia, asubuhi kulipokucha akawaambia nduguze muda umefika mie naenda maana nimewaomba mno waniache wamegoma mie naenda sasa, akakoroma na kufariki dunia.


…Sasa kilicholeta shida ni mwenyekiti wa mtaa akalazimisha ndugu kuwa mwili uletwe nyumbani uagwe then urudishwe mochwari  halafu ndiyo mwili usafirishwe kwenda kwao Moshi…basi ndugu wakawa hawataki mwili uletwe nyumbani siku bali siku inayofuata….”,anasimulia Agnes Lema.


“Emilian amekufa katika mazingira ya utata ugonjwa wake haujulikani,tunaambiwa amefariki kwa kuumwa kichwa na shingo, na kipindi anaumwa tulipokuwa tunakuja kumsalimia hapa nyumbani kwake, ndugu zake walituzuia hakuna mtu yeyote kumuona, ndipo tarehe 19 mwezi huu tukasikia amefariki, halafu sasa  hivi  tusimuage  tulipewa taarifa ya nini” ,anaeleza shuhuda mwingine aliyejulikana kwa jina la Nyorobi.


Kufuatia tukio hilo Mwenyekiti wa mtaa huo wa mtaa huo Fatuma Juma aliutangazia umma kuwa familia ya marehemu imepigwa faini ya shilingi 500,000/= kwa kucheza na akili za wanazengo.


Inaelezwa kuwa Emilian amefariki kwa kuumwa kichwa na shingo na kwamba ameacha mjane na mtoto mmoja Neema Kulwa(01), na tayari Mwili wake umesafirishwa leo kwenda Moshi kwa ajili ya mazishi.


Hata hivyo taarifa zilizoifikia Malunde1 blog ni kwamba ndani ya familia ya marehemu kuna mmoja anatuhumiwa kuwa ni mchawi  na jamii imejawa na imani za kishirikina kuwa huenda ndiyo amemtoa kafara kijana huyo ambaye ni mtoto wa dadake.
Malunde1 blog bado inafuatilia kwa undani kuhusu tukio hili..tutawaletea habari zozote tutakazozipata..

Manispaa ya Shinyanga ni miongoni mwa maeneo ambayo baadhi ya watu wake wanaimani za kishirikina, ni hivi karibuni tu watu wawili walifariki dunia katika mazingira ya kutatanisha kwa kile kilichodaiwa kuwa walifariki kwa shoti ya umeme kwenye nyumba isiyo na umeme vifo ambavyo mpaka sasa chanzo chake hakijulikani.

Na Marco Maduhu na Malunde1 blog Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527