Picha!! RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA WAZIRI MKUU MSTAAFU SUMAYE WA CHADEMA HOSPITALINI ALIPOLAZWA


Tangu juzi kumekuwa na ripoti mfululizo kwenye vyombo vya habari kuhusu kuumwa na kulazwa kwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye katika hospitali ya Muhimbili Leo Rais Magufuli amefunga safari kuelekea katika hospitali ya Muhimbili kwenda kumjulia hali mzee Sumaye japokuwa hata yeye mwenyewe hakuwa na taarifa ya ujio wa ugeni wa Rais.
"Nimeshukuru sana Rais kuja kunitembelea hapa ni jambo kubwa, nimeshtuka kwa sababu sikutegemeana sikupata taarifa yoyote…. namshukuru Rais Magufuli kwa upendo wake, anaonesha kujali sana watu wake." Amesema Frederick Sumaye na kuongeza;

"Naendelea vizuri, hali yangu ni nzuri natumaini baada ya muda mfupi nitatoka hospitali"
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Januari 11, 2016

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye na Mama Esther Sumaye alipokwenda kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu huyo Mhe Freredick Sumaye katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Januari 11, 2016


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post