MUME AUA MKEWE KWA KUMCHARANGA MAPANGA KISHA KWENDA POLISI KUWATAAIFU KUWA AMEUA
Kuna hii stori ya mauaji iliyotokea maeneo ya Kivule jijini Dar es salaam inahusu ugomvi wa mume na mke uliosababisha kifo cha mwanamke. 


Mwanamme huyo amemuua mke wake kisha kwenda polisi kuwaarifu kuwa amemuua mke wake.
Inaelezwa kwa baada ya kumkata mapanga mkewe mwanamme huyo alipiga deki nyumba nzima kiasi kwamba waliofika eneo la tukio hawakuona hata tone la damu ingawa mwili wa mwanamme huyo ulikuwa na majeraha makubwa.

Majirani walishuhudia ugomvi lakini hawakujua sababu ya ugomvi kwa sababu mume na mke walikuwa wanapigana huku wakijibizana kilugha. 


Majirani hao wanasema huenda ugomvi ulisababishwa na kugombea mali, kwani mume alioa mwanamke mwingine baada ya mke huyo mkubwa kudai wagawane nyumba, majibizano yakaleta ugomvi ambao ukapelekea mwanamke huyo kufariki.

Majirani wamesema mwanaume huyo alienda Polisi na kwa mjumbe yeye mwenyewe kutoa taarifa za kufanya mauaji, hakuonekana na hofu yoyote.

Unaweza kuplay hii sauti kuisikiliza Hekaheka yote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527