Mauaji ya Kutisha Katavi!! WATU WAWILI WACHINJWA KAMA KUKU WAKIWA WAMELALA MAJUMBANI MWAO USIKU



 
Watu wawili wameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na kukatwakatwa na mapanga katika sehemu mbalimbali za mwili Mkoani Katavi katika matukio mawili tofauti yaliyotokea katika vijiji vya Bindi na Mwamkulu.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Focas Malengo ameiambia Malunde1 blog kuwa tukio la kwanza lilitokea hapo juzi majira ya saa saba usiku katika Kijiji cha Ibindi Tarafa ya Nsimbo Wilayani Mlele.

Katika tukio hilo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Chalya Kishosha(60) Mkazi wa Kijiji cha Ibindi alikutwa akiwa ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na kukatwa katwa na mapanga kichwani na watu wasiojulikana wakati akiwa amelala chumbani kwake.

Alisema siku hiyo ya tukio wauaji hao walifika nyumba nyumbani kwa marehemu majira hayo ya usiku na kisha walivunja mlango na kisha waliingia ndani na kuanza kumshambulia kwa kumchinja shingo na kumkata kata kichwani kwa mapanga hadi kufa na kisha walitokomea kusiko fahamika .

Tukio jingine lilitokea January 2 Mwaka huu katika Kitongoji cha Center John Kijiji cha Mwamkulu Wilaya ya Mpanda, ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Tiho Robert (40) alikutwa akiwa ameuaawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na kukatwa katwa na mapanga kichwani na mkono wake wa kulia na watu wasiofahamika.

Kamanda Focas amesema mtu huyo alivamiwa na wauaji hao wakati akiwa amelala ndani ya nyumba yake majira ya saa kumi na nusu usiku.

Kaimu Kamanda Focas Malengo alisema wauaji hao ambao bado hawajafamika baada ya kutekeleza mauaji hayo walikimbia na kutokomea kusiko julikana.

Alisema chanzo cha mauaji hayo ya kikatili na ya kutisha bado hakijajulikana na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wa vijiji vya Mwamkulu na Ibindi wanaendelea kufanya msako ili kuweza kuwabaini waliohusika na mauaji ya watu hao.
 Na Walter Mguluchuma-Malunde1 blog Katavi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527