KUHUSU TAARIFA ZA KIFO CHA MWANDISHI WA KITABU CHA NGOSWE ,PENZI KITOVU CHA UZEMBEMwandishi maarufu wa tamthilia na kitabu cha ‘Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe’, Edwin Semzaba amefariki jana.


Mbali na kuwa mwandishi maarufu, Semzaba alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia, alikuwa mwenyekiti wa Umoja Wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA).


Semzaba ambaye kitabu chake cha Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe kilimpatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, aliwahi kueleza kuwa alianza kuandika kitabu hicho akiwa anasoma kidato cha pili akiwa na umri wa miaka 16 tu.


Aliimalizia kazi yake hiyo nzuri baadae ambapo ilikubalika na kuanza kurushwa kupitia Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na baadae kuiweka katika kitabu kilichokubalika na kutumika kama kitabu cha kiada kwa shule za sekondari.

Tunatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na taifa kwa ujumla. Apumzike kwa amani, Amina!

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post