HOUSE GIRL AJINYONGA KWA KUTUMIA MTANDIO HUKO MUSOMA


Mfanyakazi wa ndani anadaiwa kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia mtandio kwenye nyumba ya mwajiri wake iliyopo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.


Ofisa Mtendaji wa Kata ya Iringo, Asia Temu alisema mfanyakazi huyo alijiua hivi karibuni bila ya kuacha ujumbe wowote kuhusiana na sababu za kuchukua uamuzi huo.


Temu alisema tukio hilo liligundulika baada ya mtoto mdogo wa mfanyakazi huyo aliyemtaja kwa jina la Zatila Said kuhitaji huduma kutoka kwa mama yake na kuanza kulia kwa kutomuona.

Alisema kutokana na hali hiyo, mtoto wa mwenye nyumba, Wendelini Dominick (8) alichukua jukumu la kumtafuta mfanyakazi huyo ndani ya nyumba yao na kumkuta amekufa kwa kujinyonga.


Mwajiri wa mfanyakazi huyo, Dominick Papaa alisema alijinyonga wakati akiwa kazini na mkewe.


Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Phillip Kalangi alisema hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo na kusisitiza wanafanya uchunguzi kubaini chanzo chake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527