HII NDIYO PICHA YA RAIS MAGUFULI ITAKAYOANZA KUTUMIKA KATIKA OFISI MBALIMBALI,ATAKAYEICHAKACHUA ATAKIONA CHA MOTO


Picha Rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli itaanza kuuzwa Januari 08, 2015, katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) Mtaa wa Samora.



Kila nakala ya picha hiyo itauzwa shilingi Elfu Kumi na Tano tu bila fremu. Picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere itauzwa shilingi Elfu Tano tu. Aidha, Picha hizo zitauzwa katika Ofisi za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA). 


Picha hizo zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali, Taasisi za Umma, Mashirika na Ofisi binafsi. Kila ofisi inatakiwa iwe na picha ya Mhe. Rais pamoja na Baba wa Taifa. 



Serikali inatoa onyo kwa wale wote wanaosambaza picha isiyo rasmi pamoja na Serikali kutoa taarifa kusitisha matumizi ya picha hiyo na wanaotengeneza picha ukubwa ambao siyo rasmi.


Hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Idara ya Habari(MAELEZO) ndio yenye Haki miliki ya picha hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527