BAADA YA MNYAMA SIMBA KUCHINJWA BILA HURUMA....YANGA NAYO YATUPWA KULE, URA YA UGANDA YAWATWANGA BILA HURUMA





Saa chache baada ya mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2016 kumalizika, kwa klabu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani kuibuka na ushindi wa goli 1-0 na kuweka rekodi ya kucheza fainali yake ya tano ya michuano hiyo.

Usiku wa January 10 klabu ya Dar Es Salaam Young African nayo ilishuka dimbani kucheza mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya klabu ya URA ya Uganda katika dimba la Amaan, mchezo ambao ulikuwa unamtafuta bingwa mmoja kati ya timu hizo kwenda kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika hatua ya fainali ya michuano hiyo.

Yanga ambayo ilikuwa inaongoza katika msimamo wa Kundi A ilianza kwa kupachika goli la uongozi dakika ya 13 kupitia kwa Amissi Tambwe ambaye aliutumia vyema mpira uliopigwa kichwa na Simon Msuva na kushindwa kutinga nyavuni, kipindi cha pili URA waliendelea kuwa na nidhamu ya mchezo, licha ya kuwa walikuwa nyuma.

URA walifanikiwa kupata goli la kusawazisha dakika 14 kabla ya mchezo kumalizika kupitia kwa Peter, hadi dakika 90 zina malizika Yanga 1-1 URA. Katika hatua ya mikwaju ya penati Geofrey Mwashiuya na Malimi Busungu walikuwa hawana bahati, kwani walikosa penati, lakini URA mchezaji aliyekosa penati alikuwa ni Sekito Sam pekee. URA imeifuata Mtibwa Sugar fainali kwa kuibuka na ushindi wa penati 4-3.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527