AHUKUMIWA MIAKA MITANO JELA KWA KUIBA NG'OMBE HUKO KATAVIMahakama ya Wilaya ya Mpanda imemuhukumu John Ngasa (32) Mkazi wa Kijiji cha Mwamkulu Wilaya ya Mpanda kutumikia jela kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kuiba Ng’ombe mbili zenye thamani ya shilingi laki mbili.

Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Odira Amwol mara baada ya kulizika na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka uliokuwa na mashahidi watano.

Awali katika kesi hiyo Mwendesha Mashitaka Kulwa Kusekwa alidai kuwa Ngasa alitenda kosa hilo Aprili 25, 2015 majira ya saa mbili usiku huko katika Kijiji cha Mwamkulu Wilayani Mpanda.

Siku hiyo ya tukio mshitakiwa anadaiwa kukamatwa akiwa ameiba Ng’ombe wawili wa mwanakijiji mwenzake aitwaye Madirisha Msalaba zenye thamani ya shilingi laki tisa .

Mwendesha Mashitaka Kulwa alidai kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuiba Ng’ombe hao alianza kuwaswaga kwa ajiri ya kuwapeleka eneo jingine hata hivyo wakati akiwa bado njiani Askari wa jadi(Sungusungu) wa Kijiji hicho walipata taarifa ya kuibiwa kwa Ng’ombe hao na ndipo walipofanikiwa kumkamata mshitakiwa Ngasa akiwa na Ng’ombe hao wawili.

Katika utetezi wake Ngasa ambae hakuwa na shahidi hata mmoja huku upande wa mashitaka ukiwa mashahidi watano alikana kuiba Ng’ombe hizo .

Hakimu Odira Amwol kabla ya kusoma huku aliiambia Mahakama kuwa mshitakiwa amepatikana na hatia ya kuiba Ng’ombe wawili kutokana na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka hivyo mshitakiwa anapewa nafasi ya kujitetea kama unasababu yoyote ya msingi ya kuiomba Mahakama impunguzie adhabu .

Mshitakiwa Ngasa katika utetezi wake aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa Mama yake mzazi pamoja na wadogo zake wanamtegemea yeye .

Utetezi huo ulipigwa vikali na Mwendesha Mashitaka Kulwa ambae aliiomba Mahakama itowe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Hakimu Amwol alisoma ukumu na kuiambia Mahakama kuwa mshitakiwa John Ngasa amahukumiwa na Mahakama hiyo kwenda kutumikia jela kifungo cha miaka mitano jela kuanzia jana na kama haja lidhika na hukumu hiyo anayonafasi ya kukata rufaa.
 
Na Walter Mguluchuma-Malunde1 blog Katavi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527