

Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati wakiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita na kurudi kijijini Msoga. Kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

Rais Mstaafu Kikwete akiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu. Kushoto kwake ni Rais Magufuli

Rais Magufuli akimsindikiza Rais MstaafuKikwete.

Rais Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu Kikwete na mkewe, Salma.

Wakielekea kwenye helikopta itayowachukua hadi kijijini Msoga

Picha ya pamoja kabla safari ya Msoga kuanza

Rais Magufuli akiagana na Rais Mstaafu Kikwete

Rais Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo na watumishi wa Ofisi ya Rais wakiagana na Rais Mstaafu Mrisho Kikwete
Social Plugin