Picha 70 !! SHUHUDIA HAPA MAHAFALI YA NNE SHULE YA LITTLE TREASURES SHINYANGA

Hapa ni katika geti la Shule ya Little Treasures iliyopo katika kijiji cha Bugayambele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.Pichani ni wahitimu 82 wa darasa la awali (Pre Unit) mwaka 2015 wakiandamana kutoka Mwasele kupitia Shycom kisha katika shule hiyo ikiwa ni mahafali ya 4 katika shule hiyo ya Msingi iliyoanzishwa mwaka 2011 ikiwa na wanafunzi wanne pekee na sasa ina jumla 452.

 
Mamia ya wazazi na walezi wa wanafunzi hao wamehudhuria mahafali hayo..Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde hakupitwa na tukio hilo...ametuletea picha 70 kuanzia mwanzo hadi mwisho..Tazama hapa chini


Maandishi katika moja ya jengo la shule ya msingi Little Treasures

Wahitimu wa shule ya awali katika shule ya Little Treasures wakielekea ukumbini wakitokea katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.Shule ya Little Treasures imejizolea umaarufu mkubwa kutokana na kuwa na mazingira rafiki ya kujifunzia kwa watoto hali inayosababisha watoto kupata elimu bora inayoendana na sayansi na teknolojia.

Shule ya Little Tresures inafundisha masomo ya Kiingereza,Kifaransa,Kiswahili na ujasiliamali ikiwemo ufugaji wa samaki,ng'ombe wa kisasa

Maandamano yanaendelea

Wahitimu wa shule ya awali wakiandamana

Wapiga matalumbeta maarufu mjini Shinyanga wakifanya yao

Askari wa kitengo cha usalama barabarani akiwaongoza wahitimu wa shule ya awali(Pre Unit) wakati wa maandamano yao leo

Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiandamana kuelekea ukumbi wa sherehe katika eneo la shule hiyo iliyopambwa kwa maua na miti

Maandamano yanaendelea

Wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la Tano wakiwa katika maandamano kuwasindikiza wenzao waliomaliza masomo ya awali(Pre Unit) wanaojiandaa kuanza masomo ya darasa la kwanza mwaka 2016

Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akiwa na mgeni rasmi katika mahafali hayo ya 4 bi Happiness Mrangi kutoka TRD kwa niaba ya afisa elimu mkoa wa Shinyanga(katikati),kulia kwake ni mkurugenzi wa shule ya Little Tresures Lucy Dominic wakielekea katika eneo palipokuwa panafanyika sherehe za kuwaaga wanafunzi wa shule ya awali.

Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akiongoza msafara wa wageni waalikwa katika mahafali hayo

Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akiwakaribisha wageni waalikwa,wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wakati wa mahafali ya 4 ya wanafunzi wa shule ya awali katika shule hiyo,ambapo alisema ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha mtoto anapata haki ya elimu kwa ndiyo urithi pekee wa uhakika katika maisha yao

Wazazi wa wahitimu wakiwa ukumbini

Wazazi wakiwa eneo la tukio

Sherehe inaendelea

Wazazi wakiwa eneo la tukio

Tunafuatilia kinachojiri hapa.....


Mgeni rasmi Happiness Mrangi akizungumza katika mahafali hayo ambapo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi na walezi umuhimu wa kupeleka watoto shule,huku akihamasisha watumie shule hiyo kwani ina walimu wazuri,mazingira mazuri ya kujifunzia lakini pia shule ina usafiri ambao huutumia kuwasafirisha wanafunzi kutoka majumbani hadi shuleni kila siku.Kushoto kwake ni mwalimu mkuu wa shule ya Little Treasures Paul Kiondo,kulia ni mkurugenzi wa shule hiyo Lucy Dominic




Wazazi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea eneo la tukio



Ukafika muda wa burudani-Wahitimu wa shule ya awali wakiimba



Wahitimu wakiimba kwa lugha ya kiingereza,moja ya nyimbo zao ilikuwa ni kuhamasisha jamii kupiga vita rushwa na wazazi kuthamini elimu


Wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Little Treasures wakiimba na kucheza



Naely Mrindoko akisoma risala kwa niaba ya wanafamilia wa shule ya msingi Little Treasures,pamoja na mambo mengine alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 452 ikiwa ni pamoja na wale wanaosoma katika shule ya msingi ya Mwasele.Shule hiyo pia ina walimu 14 waliobobea,watumishi 22,magari 9 kwa ajili ya wanafunzi na watumishi,pikipiki 1,madarasa 8,vyoo 22 na kwamba hivi sasa wanajenga bweni la kisasa kwa ajili ya wanafunzi ili kupunguza gharama za kusafirisha wanafunzi kila siku



Wanafunzi wa darasa la pili wakichora umbo la ramani ya shule ya msingi Little Tresures



Wahitimu wakishuhudia burudani kutoka kwa kaka na dada zao wa darasa la pili


Mahafali yanaendelea



Wanafunzi wa darasa la tatu wakicheza ngoma ya Kikurya

Watoto wakicheza ngoma ya asili ya Kikurya

Wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la Tano wakiwa eneo la tukio

Wahitimu wakiwa eneo la tukio

Mahafali yanaendelea

Tunafuatilia kinachoendelea hapa

Wageni waalikwa wakiwa eneo la tukio

Tunasikiliza na kuangalia kinachoendelea

Wazazi na walezi wa wanafunzi wakiwa eneo la tukio

Tunafuatilia kinachoendelea hapa

Wageni waalikwa wakiwa eneo la tukio

Wanafunzi wa darasa la nne wakitoa burudani

Sherehe inaendelea

Wahitimu katika pozi

Wanafunzi wakiroa burudani

Tunaangalia burudani

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akiwahamasisha wazazi kupeleka watoto wao katika shule hiyo kwani hakuna gharama kubwa huku akiwashukuru wazazi na jamii inayowazunguka kwa ushirikiano wao katika kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu bora

Wageni wengine waliamua kukaa chini ya mti kwani shule hiyo ina miti mingi na wamejiwekea utaratibu wa kupanda miti kila tarehe 1 mwezi Novemba ambapo wazazi hufika katika shule hiyo na kupanda miti

Tunafuatilia kinachoendelea

Wageni waalikwa wakiwa eneo la tukio

Wazazi wakiwa eneo la tukio

Wanafunzi wa Middle Class wakitoa burudani

Wazazi wakiwa eneo la tukio

Wazazi wakiwa wamebeba zawadi kwa ajili ya watoto wao

Wanafunzi wa darasa la Tano ambao ndiyo waasisi wa shule ya msingi Little Treasures wakiimba

Sherehe inaendelea

Wanafunzi wa darasa la tatu wakionesha fashion

Tunafuatilia burudani

Wanafunzi wa darasa la Tatu wakionesha mchezo wa Fashion wakitembea Kimiss

Mgeni rasmi Happiness Mrangi akitoa hotuba yake...kulia kwake ni mkurugenzi wa shule ya Little Treasures Lucy Dominic

Wanafunzi wakiwa eneo la tukio

Wageni waalikwa wakiwa eneo la tukio

Meza kuu wakiwa wamesimama wakati wa Harambee kuchangia ujenzi wa Bweni la wanafunzi katika shule hiyo,kushoto ni mwenyekiti wa bodi ya Shule bwana Chipeta William,kushoto ni meneja wa shule hiyo Mwita Nchagwa

Meza kuu wakiwa wamesimama,kushoto ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Paul Kiondo

Wazazi wakiwa shule ya Little Treasures

Meneja wa shule ya msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akiwashukuru watu wote wenye mapenzi mema waliofika katika mahafali hayo pamoja na kuwakaribisha wazazi na walezi kupeleka watoto wao ili wapatiwe elimu bora

Watoto wakijiandaa kupokea vyeti vya kuhitimu masomo ya shule ya awali

Mzazi akiwa na mwanaye baada ya kupokea cheti

Mtoto akionesha cheti chake

Wazazi katika pozi na mtoto

Picha ya kumbukumbu

Picha ya kumbukumbu na mhitimu

Mzazi akiwa na mwanaye---Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527