MTOTO AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KISIMANI HUKO MBEYA







Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.

Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba Promis Dank mkazi wa bwawani wilaya ya Chunya amefariki dunia njiani akiwa anapelekwa hospitali baada ya kutumbukia kisimani.


Tukio hilo limetokea Novemba 11 majira ya saa 12 asubuhi huko kitongoji cha Railway, kata ya Bwawani, wilaya ya Chunya, mkoa wa Mbeya.

Inadaiwa kuwa, mtoto huyo baada ya kutumbukia kwenye kisima hicho ambacho kilikuwa wazi, aliokolewa akiwa hai lakini alifariki dunia akiwa njiani kuelekea hospitali teule ya Mwambani kwa matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwa makini hasa kwa kuweka uangalizi wa kutosha kwa watoto wadogo ili kuepuka madhara yanayoweza kuepukika.

Aidha anatoa wito kwa jamii kufunika visima vilivyowazi, kufukia mashimo yenye maji kwani ni hatari kwa watoto wadogo hasa katika msimu huu wa mvua za vuli.


Na Emanuel Madafa-Mbeya

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post