HAYA NDIYO MAAMUZI MENGINE YA RAIS MAGUFULI KUHUSU MADUDU BANDARINI BAADA YA ZIARA YA WAZIRI MKUU LEOLeo Waziri mkuu Majaliwa Kassim amefanya ziara ya kushtukiza bandarini na kuwasimamisha kazi maofisa watano kutoka katika vitengo mbalimbali kutokana na upotevu wa makontena 349 ambayo thamani ya kiasi cha shilingi 80 bilioni.


Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade

Baada ya Waziri mkuu kufanya maamuzi hayo Leo rais Dk Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna wa Mamlaka ya TRA, Rished Bade na kumteua Bwana Philip Mpango kukaimu nafasi hiyo kufuatia upotevu huo.

Taarifa nyingine kutoka Ikulu hii hapa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post