Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HASHEEM RUNGWE KWENDA MAHAKAMA KUU KWA AJILI YA TUME YA UCHAGUZI TANZANIA



Wakati tukizisubiria saa chache zijazo  kwa ajili ya kushuhudia tukio la kitaifa la kuapishwa kwa rais mteule wa Tanzania kwa awamu ya tano DK. John Pombe Magufuli,nakusogezea hii stori kutoka kwa aliyekuwa mgombea urais nchini kupitia chama cha “CHAUMA” Hasheem Rungwe ambaye amepanga kufungua kesi mahakama kuu ili iweze kutoa tafsiri ya nguvu ya tume ya uchaguzi kutohojiwa au kupelekwa mahakamani.


‘Mahakama itupe tafsiri ya sheria, wanamaana gani kwa kutuzuia kuihoji tume.? Demokrasia haikubaliani na hali hii, watu lazima waende mahali na vyombo vyenye mamlaka kutoa maamuzi viseme, hatuwezi kukaa kimya’ – Hasheem Rungwe

‘Sisi tunaenda mahakamani, kuomba mahakama iingilie kati ili watu wajue na tupate majibu” ;-Hasheem Rungwe

Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Hasheem Rungwe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com