Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga kwenye mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)/UKAWA ukiongozwa na makamu mwenyekiti wa Chadema kutoka Zanzibar Said Issa Mohamed,mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi,aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam John Guninita pamoja na viongozi mbalimbali wa UKAWA.Mkutano huo ulipaswa kuongozwa na mgombea mwenza wa Urais wa UKAWA Haji Duni lakini alipata udhuru na kutohudhuria mkutano huo...Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha 20 za mkutano huo...Angalia hapa chini....
Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini kupitia Chadema Patrobas Katambi akiteta jambo na makamu mwenyekiti wa Chadema Said Issa Mohamed
Wananchi waliohudhuria mkutano huo wakishangilia.....
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinajiri eneo la mkutano
Jukwaa kuu,viongozi mbalimbali wa Ukawa wakifuatilia kilichokuwa kinajiri eneo la mkutano
Mkutano unaendelea
Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam John Guninita akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine aliwaomba watu wote wenye kiu ya mabadiliko waliobaki ndani ya CCM watoroke waende Ukawa kwani kwa hali ilivyo sasa lazima kuwe na mabadiliko nchini Tanzania na tayari waliokuwa makada wakubwa wa CCM walishatimkia Ukawa kwa ajili ya kusaka mabadiliko ya kweli.
John Guninita aliwataka watanzania kuchagua viongozi wa Ukawa katika uchaguzi mkuu ujao kwa vile CCM imeshindwa kuwakomboa Watanzania na badala yake viongozi wachache ndiyo wananufaika na rasilimali za nchi
Bango linalosomeka "Kumtukana Lowassa ni Marashi kwa Malofa"
Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini kupitia Chadema Patrobas akiwahutubia wakazi wa Shinyanga waliojitokeza katika viwanja vya Shycom kusikiliza sera za Ukawa ambapo alisema njia pekee ya kuleta mabadiliko katika nchi ya Tanzania ni kuiondoa CCM madarakani
Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi akizungumza na wakazi wa Shinyanga na kuomba ridhaa ya watanzania wamchague mheshimiwa Edward Lowassa kuwa rais wa nchi ya Tanzania kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kweli
Mkutano unaendelea
Wananchi wakinyoosha mikono kuonesha kuwa wapo tayari kwa mabadiliko na Lowassa
Mkutano unaendelea
Makamu mwenyekiti wa Chadema kutoka Zanzibar Said Issa Mohamed akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alitumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kudumisha amani huku akilipongeza jeshi la polisi nchini kwa kuendelea kulinda amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu
Makamu mwenyekiti wa Chadema kutoka Zanzibar Said Issa Mohamed akiwahutubia wakazi wa Shinyanga
Mkutano unaendelea
Makamu mwenyekiti wa Chadema kutoka Zanzibar Said Issa Mohamed akitoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kupiga kura siku ya uchaguzi Oktoba 25,2015
Makamu mwenyekiti wa Chadema kutoka Zanzibar Said Issa Mohamed akiwa na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi jukwaani
Makada wa Chadema wakifuatilia kilichokuwa kinajiri kwenye mkutano huo....
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Social Plugin