News Alert!! BAADA YA UCHAGUZI KUFUTWA ZANZIBAR..HAYA NDIYO MAAMUZI KUHUSU UCHAGUZI TANZANIA BARA....UKAWA WAPIGILIA MSUMARI


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa kufutwa kwa uchaguzi mkuu Zanzibar hakutaathiri uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu NEC na NEC wanaongozwa na katiba mbili tofauti.


Lubuva ametoa kauli hiyo leo jioni ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuendelea na utangazaji wa matokeo ya Rais.


"NEC inapenda kuwatangazia wananchi kuwa kuhairishwa kwa uchaguzi Zanzibar hakutasababisha kuhairishwa kwa uchaguzi Tanzania.

"Uchaguzi wa Zanzibar unasimamiwa na ZEC na uchaguzi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani unasimamiwa na NEC, ni katiba mbili tofauti
"Uvumi unaoendelea kwamba uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umefutwa ni upotoshaji na si kweli, haujaathiriwa na lolote.

"Tuko hapa muda huu kuendelea na utoaji wa matokeo ya awali kama ambavyo tumekuwa tukifanya." Alisema Lubuva na kuendelea na zoezi la kutangaza matokeo hayo.

UKAWA Wapigilia msumari
Akizungumzia sakata la uchaguzi mkuu kufutwa huko Zanzibar,Mwenyekiti mwenza wa Ukawa,James Mbatia amesema kuwa tume ya uchaguzi ZEC imeamua kuyafuta matokeo hayo baada ya CCM kushindwa vibaya.

"ZEC wameamua kuufuta uchaguzi mkuu Zanzibar kwa shinikizo la serikali ya Kikwete na CCM yake baada ya Maalim Seif Sharif Hamad kuibuka kidedea.

"Huwezi kufuta uchaguzi wa Zanzibar ukaacha uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano

"Unaposema Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ni Tanganyika na Zanzibar

"Upande mmoja wa Jamhuri ya muungano umefuta uchaguzi, tena wametamka kufuta uchaguzi mkuu.Sasa kama upande mmoja umeshafuta, upande mwingine unasubiri nini?

"Huu ni mgogoro mkubwa. Kitendo cha Damian Lubuva kuendelea kutangaza matokeo ni sawa na kiini macho, anajifurahisha tu mwenyewe na ni kinyume cha katiba." Amesema James Mbatia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527