Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LOWASSA AVUNJA UKIMYA- AIPA ONYO TUME YA UCHAGUZI TANZANIA





Mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema, anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Edward Lowassa ameitaka tume ya uchaguzi kuhakikisha inafanya shughuli zake kikamilifu na bila kupendelea upande wowote kwani kushindwa kufanya hivyo ni kuliingiza taifa kwenye machafuko.


Mgombea huyo wa nafasi ya urais Edward Lowassa ametoa onyo hilo kali kwa tume ya uchaguzi nchini katika siku yake ya mwisho ya kampeni kanda ya ziwa.



Wakati siku za kuelekea Oct 25 zikizidi kuhesabika kwa haraka zaidi, Freeman Mbowe ni mwenyekiti wa Chadema taifa ambaye amesema watakaa umbali wa mita 200 kutoka kwenye vituo vya kupigia kura, wasubiri matokeo yatangazwe hata kama ni kesho yake asubuhi.

Uchaguzi wa Tanzania unatazamwa na dunia kwa jicho la tatu kwasasa,

Viongozi wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA wakiongozwa na mgombea nafasi ya urais Edward Lowasa wametuma salama za rambi rambi kwa familia Dkt Emanuel Makaidi aliyefariki dunia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com