
Haya ndiyo mabaki ya ndege iliyotoa uhai wa mgombea ubunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe,rubani wa chopa hiyo William Silaa na abiria wengine wawili ambao bado hawajajulikana ni akina nani kutoka na watu wote waliokuwa ndani ya helkopta hiyo kuungua vibaya na kutotambulika.Miili ya marehemu imepelekwa jijini Dar es salaam katika hospitali ya Lugalo


Mgombea urais wa Chadema Edward Lowassa amlilia Deo Filikunjombe....
"Ni taarifa ya kushtusha sana ya msiba wa mwanasiasa chipukizi na jasiri, Deo Filikunjombe kutokana na ajali ya Helikopta juzi jioni maeneo ya mbunga ya Selous mkoani Morogoro.
Ni pigo jingine kubwa ambalo katika kipindi kifupi Taifa limepata, huku bado likiwa na kidonda cha kuondokewa na wana siasa wengine mahiri,Marehemu Celina Kombani, Dr Abdallah Kigoda na Dr Emanuel Makaidi aliyefariki Oktoba 15,2015.
Filikunjombe alikuwa Mbunge mahiri aliyesimama imara kutetea maslahi ya wananchi wa jimbo lake la Ludewa na watanzania kwa ujumla.
Alikuwa mwiba kwa serikali ya Chama chake CCM kutetea maslahi ya nchi, mfano ni katika kashfa ya Escrow ambapo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati iliyochunguza kashfa hiyo.
Mwenyezimungu awape moyo wa subira, familia, jamaa, marafiki na wananchi wa Ludewa, katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE"Edward Ngoyai Lowassa
Deo akiwa na Lowassa enzi za uhai wake
Mke wa marehemu Deogratias Filikunjombe, Sarah Filikunjombe (kushoto) akilia kwa uchungu baada ya kupata tarifa za kifo cha mumewe.
Ndugu, jamaa na marafiki wakionekana wenye huzuni nyumbani kwa Deogratias Filikunjombe.
Nyumbani kwa Deogratias Filikunjombe Mbagala Kijichi, Dar es Salaam(hii ndiyo nyumba yake
Capt. William Silaa enzi za uhai wake.
Filikunjombe akiwaaga wananchi wake enzi za uhai wake.
Mbunge wa Ludewa Mhe. Deogratias Haule Filikunjombe amefariki dunia katia ajali ya Chopa katika hifadhi ya wanyama ya Selous, pamoja na rubani Kepteni William Silaa mfanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Wengine waliofariki kwenye ajali hiyo ni Vitalis Blanka haule na Ofisa Tawala wa Wilaya ya Tarime, Bw. Egdi Mkwera ambaye alikuwa mtaalam wa mifugo.
Picha hapo chini ni Chopa iliyosababsha kifo cha Filikunjombe, Capt. William Silaa na watu wengine wawili.
Huyu Ndo Mke wa Marehemu Mbunge Deo Filikunjombe Aliyefariki Kwenye Ajali ya Helkopta ya CCM
Social Plugin