Hii Kali!! WALIMU WANNE WAJIUA KISA WAMEKOSA MSHAHARA



Kulikuwa na ripoti mfululizo kuhusu ishu ya migomo ya Walimu Kenya wakidai nyongeza ya mishahara… hiyo ni moja ya stori ambayo imeripotiwa sana wiki chache zilizopita.


Moja wa mabango yaliyobebwa ba Walimu wakiwa kwenye mgomo Kenya.

Chama cha Walimu Kenya kimeifikisha taarifa kwenye Vyombo vya Habari kwamba walimu wanne ambao ni wanachama wa chama hicho, KNUT wamejiua kwa kujinyonga wakidai madai yao ya kulipwa mshahara wao wa mwezi September kipindi ambacho Walimu hao walikuwa wamegoma.

“Wanachama wetu wanaishi kwenye hali ngumu sana, hiyo imesababisha wengine wajiue” >> hiyo ni nukuu ya alichokisema John Mathiangi, Mhasibu wa Chama cha Walimu KNUT.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527