HAYA HAPA MATOKEO YA UDIWANI KATA ZOTE 17 ZA MANISPAA YA SHINYANGA...CCM WAPATA KATA 12...CHADEMA WAAMBULIA 4



Aliyekuwa naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila,ambaye amefanikiwa kutetea kata yake ya Ndembezi kwa kupata kura 4302 kati ya kura 6907 zilizopigwa huku mgombea udiwani wa Chadema Rojaz Mshana akipata kura 2414,Manyonyi Magoti wa ACT Wazalendo akipata kura 56 na Joyce Tambwe wa APPT Maendeleo akipata kura 10(picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog)


Aliyekuwa meya wa manispaa ya Shinyanga katika baraza la madiwani la manispaa ya Shinyanga lililopita,Gulam Hafeez Mukadam ambaye pia amefanikiwa kutetea kata yake ya Shinyanga mjini(picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog)
*******
Chama cha Mapinduzi katika manispaa ya Shinyanga kimeibuka na ushindi nafasi ya udiwani katika kata 12 kati ya 17 huku Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikipata ushindi katika kata tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 kote nchini.

Miongoni mwa kata zilizonyakuliwa na CCM ni kata ya Shinyanga mjini iliyokuwa inatetewa na aliyekuwa meya wa manispaa hiyo Gulam Hafeez Mukadam na kata ya Ndembezi iliyokuwa inatetewa na aliyekuwa naibu meya wa manispaa hiyo David Nkulila.

Hata hivyo Chadema wamefanikiwa kutetea kata 4 kati ya 6 zilizokuwa zinaongozwa na madiwani wa Chadema katika baraza la madiwani lililopita ambazo ni Ndala,Masekelo,Kitangiri na Ngokolo huku wakipoteza kata ya Ibadakuli na Kambarage na kupata ushindi katika kata ya Lubaga.

Kata zilizonyakuliwa na CCM ni Ndembezi,Shinyanga Mjini,Old Shinyanga,Ibinzamata,Kolandoto,Mwamalili,Chibe,Mwawaza,Ibadakuli,Kambarage,Chamaguha na Ibadakuli.

Chadema wamepata ushindi katika kata ya Ndala,Masekelo,Kitangiri,Lubaga na Ngokolo.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527