Tanzia!! WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ABDALAH KIGODA AFARIKI DUNIA
Monday, October 12, 2015
Waziri wa viwanda na biashara ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Handeni Dr.Abdalah Kigoda amefariki dunia leo majira ya saa 10 jioni nchini India wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Appolo.
Waziri huyo amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Apollo nchini India
Siku chache zilizopita waziri Kigoda alizushiwa kifo katika mitandao ya kijamii jambo lililokanushwa vikali na serikali kupitia kwa masemaji wake Bw Assah Mwambene
Dkt Kigoda ni waziri wa pili kufariki katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu baada ya waziri Celina Kombani naye kufariki dunia mwezi uliopita katika hospitali hiyo hiyo ya Apollo ya India alikokuwa akipatiwa matibabu
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin