Breaking News!!! MATOKEO YOTE YA UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR YAMEFUTWA...SABABU 9 ZIKO HAPATume ya Uchaguzi Zanzibar imeufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar kutokana na kuwa na dosari nyingi ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru na wa haki .


Mwenyekiti wa ZEC amewaambia waandishi wa habari mchana huu kuwa amechukua maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa uchaguzi uligubikwa na dosari nyingi.

"Mimi nikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, nimeridhika kuwa Uchaguzi huu umegubikwa na makosa makubwa....

"Kwa mamlaka niliyonayo natangaza rasmi kuufuta uchaguzi huu kwa kuwa haukuwa huru na wa haki, mtajuulishwa tarehe itakayofanyika uchaguzi mwengine hapo baadae, Ahsanteni kwa kunisikiliza"! - Jecha S. Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post