
Msafara wa Mhe. Edward Ngoyai Lowassa ukiwa umezingirwa na umati watu wa Musoma akielekea uwanja wa Mkendo Musoma,Jumapili 11/10/2015

Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (Kulia) na Mhe. Vicent Nyerere wakiwasili katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo Musoma leo Jumapili 11/10/2015

Vicent Nyerere akiongea na wananchi wa Musoma katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo Musoma mjini,Jumapili 11/10/2015

“Wingi wenu ni ishara kubwa kuwa mnataka mabadiliko ya kweli, natambua mnayo matatizo mengi hapa, ninaombeni mtumie wingi wenu huu kunipigia kura, mbunge na madiwani ili tuweze kuleta mabadiliko, nasisitiza nipeni mgombea ubunge ili tushirikiane kukamilisha matatizo hayo ikiwamo barabara,” amesema Lowassa




















“Wanasema wewe mwizi, sisi huku tumesema tutamchagua mwizi na kumfungia Ikulu miaka 10 atumikie wananchi.”-Vicent Nyerere(Mwenyekiti wa Chadema Musoma Mjini)

“Lowassa wamekutukana sana na wengine wanasema wewe mgonjwa, sasa sisi tumesema Mkoa wa Mara tunamchagua mgonjwa ili ashughulikie masuala ya hospitali zetu kwa kuwa hilo ndilo tatizo kubwa".-Vicent Nyerere

“Rais ambaye akiweka sahihi mtu ananyongwa, sahihi yake inaruhusu nchi kuingia vitani, anazungumza kuwa atajenga Mahakama za kufunga wezi na mafisadi, wakati ukienda magereza waliojaa ni walala hoi… sisi watu wa Mkoa wa Mara tunasema hatuhitaji mahakama za mafisadi, tunahitaji hospitali bora,” alisema Nyerere.


Social Plugin