Angalia Picha 50- MDAHALO WA KUJADILI AMANI BAADA YA UCHAGUZI MKUU TANZANIA WAFANYIKA MJINI SHINYANGA



Hapa ni katika ukumbi wa Vijana Center uliopo katika kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga,ambako leo Oktoba 30,2015 kumefanyika mdahalo maalumu ulioandaliwa na Radio Faraja Fm Stereo kwa kushirikiana na BBC Media Action ukiwa na mada "Je ni nani anawajibika kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kuwepo nchini Tanzania baada ya uchaguzi mkuu".Wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali,vyama vya siasa,dini,wananchi,wanaharakati,taasisi za kiraia,waandishiwa habari na wananchi wamejadili masuala mbalimbali yatakayohakikisha amani ya nchi inaendelea kuwepo.


Wadau hao wa amani wamekubaliana kulinda amani ya nchi baada ya uchaguzi huku wakisisitiza ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa amani iliyopo inadumu.Aidha wamesema ni vyema viongozi wa dini,siasa,wanaharakati,waandishi wa habari na kila mpenda amani anaepuka vitendo vinavyoweza kusababisha vurugu…Hali kadhalika wamewataka viongozi wa siasa kuchunga ndimi zao ili kuliepusha taifa kuingia katika vurugu kwani wao ndiyo wana makundi makubwa ya vijana nyuma yao ambayo kwa asilimia kubwa yanategemea kauli za viongozi wao….. -Malunde1 blog ilikuwepo eneo la tukio..angalia picha 50 za tukio hilo....



Kushoto ni Noel Thomson kutoka BBC Media Action akiwa ukumbini,katikati ni mshariri mkuu wa Radio Faraja bwana Simeo Makoba(aliyekuwa MC katika mdahalo huo)




Wadau wakiwa ukumbini kujadili mstakabali wa taifa baada ya uchaguzi mkuu Tanzania


Waongozaji wa mdahalo huo Veronica Natalis na Steve Kanyefu wakiwa ukumbini




Washiriki wa mdahalo wakiwa ukumbini




Watangazaji kutoka Radio Faraja Fm Stereo wakiwa ukumbini




Justina Marwa wa BBC Media Action(kushoto),akifuatiwa na Nunu Abdul na Wezay Ally wakiwa ukumbini




Mwongozaji wa mdahalo huo Veronica Natalis akiwa ukumbini




Wadau wa amani wakiwa ukumbini




Meza kuu




Mwongozaji wa pili wa mdahalo huo bwana Steve Kanyefu akiwa ukumbini




Mwanasheria Penina Samwel akijitambulisha ukumbini




Mkurugenzi wa shirika la Agape mkoani Shinyanga John Myola akiwasalimia washiriki wa mdahalo huo




Mwakilishi wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Dismas Gapi Kisusi akizungumza




Wadau wakiwa ukumbini




Diwani wa kata ya Ngokolo mjini Shinyanga Ntobi Emmanuel akiwa ukimbini




Mkurugenzi wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde akiwa ukumbini




Wadau wa amani wakiwa ukumbini




Mdahalo unaendelea




Mdahalo unaendelea




Mwakilishi wa sheikh wa mkoa wa Shinyanga,Sheikh Majaliwa Masoud akiwa ukumbini




ACP Dismas Gapi Kisusi akiwa ukumbini




Kushoto ni askofu John Nkola wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga akiwa na mkurugenzi wa shirika la Agape John Myola




Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini




Kushoto ni mtangazaji wa radio Faraja Agnes Kambarage,akifuatiwa na Justina Marwa kutoka BBC Media Action,kulia ni mtangazaji wa radio Faraja Nunu Abdul



Watangazaji wa Radio Faraja Faustine Kasala(kushoto) na Magera Evarist wakifanya yao


Mkazi wa Shinyanga akizungumza



Mkazi wa Shinyanga akizungumza ukumbini




Mdahalo unaendelea




Kulia ni aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini kupitia chama cha APPT Maendeleo Elisiana Tambwe akiwa ukumbini




Mdahalo unaendelea




Mkuu wa kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Buhangija Peter Ajali akiwa na diwani mteule wa kata ya Ndembezi David Nkulila(kulia)




Mdahalo unaendelea




Mdahalo unaendelea




Mdahalo unaendelea




Askofu John Nkola akisisitiza jambo




Afisa maendeleo wa manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dosi kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga akizungumza ukumbini




Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Shinyanga Siri Yasin akizungumza




Diwani wa kata ya Ngokolo Ntobi akizungumza




Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini kupitia chama cha APPT Maendeleo Elisiana Tambwe akizungumza




Diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila akizungumza





Mchungaji wa kanisa la Gilgari mjini Shinyanga akizungumza




Mdahalo unaendelea




Mdahalo unaendelea




Mkurugenzi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde akizungumza ukumbini




Waongozaji wa Mdahalo Steve Kanyefu na Veronica Natalis wakiteta jambo ukumbini




Watangazaji wa radio Faraja,Moshi Ndugulile,Faustine Kasala,Steve Kanyefu na Veronica Natalis wakiwa ukumbini baada ya mdahalo kumalizika




Watangazaji wa radio Faraja Isack Edward,Moshi Ndugulile na Nunu Abdul wakiwa nje ya ukumbi wa mdahalo...Picha zote na wapiga picha wa Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527