Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA 18- MKUTANO WA MGOMBEA URAIS WA ACT WAZALENDO LEO SHINYANGA...CHOPA YA CCM YAWACHEFUA




Oktoba 17,2015- Hapa ni katika viwanja vya shule ya msingi Town mjini Shinyanga ambako leo mgombea urais wa Chama cha ACT Wazalendo mheshimiwa Anna Mghwira amefanya mkutano wa kampeni kuomba kura kwa wakazi wa Shinyanga na kuwanadai wabunge na madiwani wa chama hicho......Mwandishi mkuu wa mtandao huu  wa Malunde1 blo ndugu Kadama Malunde ametuletea picha 18...angalia hapa chini




Jukwaa kuu



Mgombea udiwani Kata ya Chamaguha Siri Yasin aliyekuwa kada wa Chadema kabla ya kutimkia Act Wazalendo akiomba kura kwa wananchi..Pamoja na mambo mengine Siri Yasin alieleza kukerwa na kitendo cha mgombea ubunge wa CCM jimbo la Shinyanga Stephen Masele kutumia helkopta katika kampeni zake wakati jimbo jenyewe ni dogo na kuongeza kuwa hayo ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi huku akidai kuwa kwa siku moja tu gharama za kuendesha chopa hiyo ni kubwa sana ambapo makadirio ni shilingi milioni 4 na laki 8 kwa saa moja.


Mgombea mwenza urais ACT Wazalendo Hamad Yusuph akizungumza katika mkutano huo ambapo alisisitiza kuwa kamwe hawawezi kupiga kura Oktoba 25 halafu wakalale kwani kura ni mali..




Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano




Tunafuatilia mkutano.....




Viongozi mbalimbali wa ACT Wazalendo wakiwa eneo la mkutano




Wananchi wakiwa eneo la mkutano wakifuatilia sera za ACT Wazalendo




Mgombea mwenza urais ACT Wazalendo Hamad Yusuph akisisitiza umuhimu wa wananchi kupiga kura ili kuiondoa CCM maadarakani kwani imeshindwa kuwakomboa watanzania


Baadhi ya wagombea udiwani wa ACT Wazalendo wakiwa eneo la mkutano wakijiandaa kutambulishwa



Mgombea urais Tanzania kupitia ACT Wazalendo Anna Mghwira akiwahutubia wakazi wa Shinyanga leo ambapo alieleza sera za chama chake na kuomba ridhaa watanzania wamchague kuwa rais wa nchi ili kuwainua kiuchumi na kutumia rasilimali za nchi vizuri







Wananchi wakimsikiliza mgombea urais




Mheshimiwa Anna Mghwira akizungumza mjini Shinyanga ambapo alisema viongozi wa CCM wanatumia rasilimali za nchi vibaya kwa kujinufaisha wao binafsi huku akisema ni aibu na jambo la ajabu kwa kiongozi kutumia Helkopta kufanya kampeni kwenye jimbo dogo kama la Shinyanga mjini ambapo hivi sasa mgombea wa CCM jimbo hilo Stephen Masele anasafiri kwa chopa kutoka kata moja hadi nyingine...




Mkutano unaendelea




Mkutano unaendelea




Mkutano unaendelea




Wananchi wakiwa eneo la mkutano




Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini pia mgombea udiwani kata ya Kambarage Nyangaki Nshilungushela maarufu Mzee wa Utaratibu akiomba kura kwa wananchi...Huyu pia alikuwa kada wa CHADEMA aliyeamua kuhamia ACT Wazalendo

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com