Picha_MWILI WA MAREHEMU WAZIRI CELINA KOMBANI WAWASILI NCHINI,KUZIKWA SIKU YA JUMATATU MKOANI MOROGORO


Viongozi mbalimbali wakiwa katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam tayari kwa kuupokea mwili wa marehemu Celina Kombani.


Wananchi wa mkoa wa Morogoro wamepokea kwa majonzi msiba wa aliyekuwa waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na mbunge wa jimbo la Ulanga Bi, Celina Kombani mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumatatu wiki ijayo katika eneo la shamba lake lililopo Lukobe manispaa ya Morogoro.



Wakizungumza nyumbani kwa marehemu wakazi wa Morogoro wameeleza kusikitishwa na msiba huo ambapo wamesema marehemu alikuwa kipenzi cha watu, mchapa kazi na kuwataka wakazi wa Morogoro hususani wa jimbo la Ulanga kuwa wavumilivu kwa kupotelewa na kipenzi chao ambapo waziri huyo alikuwa anagombea ubunge kwa awamu ya tatu kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Ulanga.

Wakizungumza  kwa niaba ya familia kaka wa marehemu Martin Ombeshi na mkwe wa marehemu Bw, Jeradi Mlenge wamesema wameupokea msiba huo kwa masikitiko ambapo wameeleza mazishi yatafanyika mkoani Morogoro siku ya Jumatatu shambani kwake Lukobe na msiba utapelekwa nyumbani kwao Mahenge wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527