Wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma katika vyuo vikuu viliopo bara na Zanzibar wamevamia Ofisi za bodi ya mikopo ya Zanzibar wakidai posho zao ambazo hawajalipwa kwa kipindi cha mwaka mzima na fedha za ada za masomo.
Mwandishi wa habari hizi aliwakuta wanafunzi hao wapatao 70 wamekusanyika nje ya jengo la bodi hiyo ya mikopo wakitafakari na kutafuta mbinu za kudai malimbikizo ya fedha zao za posho ambazo ni zaidi ya mwka mzima hawaajlipwa na bodi hiyo imekuwa ikitoa ahadi hewa kupata fedha hio na wameiomba seriklai ilivalie njuga suala hilo.
Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa bodi hiyo ya mikopo ya Zanzibar Bw.Idi Khamis ambaye amekiri kuwepo kwa hali hiyo ya wanafunzi ingawa amesema tatizo kubwa linakuja kuwa wanafunzi hao wenyewe hawalipi madeni yao ambapo wanadai karibu bilioni 30 huku akiwahakikishia wanfunzi hao pamoja kuwa serikali tayari imeshandaa mpango wa kulipa ada mwaka huu wanapaswakueelewa kuwa sio bodi ndio yenye malaka ya kulipa fedha zote..
Bodi hiyo ya mikopo ya Zanzibar ambayo hutegemea ruzuku serikalini na fedha za urejeshaji inahitaji shIlingi bilioni 8 kwa mwaka kwa ajili ya kuwalipia ada na posho wanafunzi wanaosoma Tanzania bara katika vyuo mbali mbali na wakiwemo wanafunzi wa Zanzibar .
Via>>ITV
Social Plugin