MWANDISHI WA HABARI ATIMULIWA KWENYE MSAFARA WA MAGUFULI...KISA HABARI YA MAGUFULI KUZOMEWA MBEYA



Mwandishi wa gazeti la MWANANCHI ndugu Peter Elias ametimuliwa kutoka msafara wa kampeni za mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ndugu John Magufuli, imethibitishwa.



Mwandishi huyo ametimuliwa kwa kosa la kuripoti tukio la mgombea huyo kuzomewa na wafuasi wa Chadema jijini Mbeya hivi karibuni kinyume cha makubaliano.

Mwandishi huyo aliripoti katika gazeti hilo kwa kichwa cha habari "Magufuli akabiliana na UKAWA Mbeya" na kuweka picha ya mgombea huyo akionyeshwa alama ya vidole viwili.

  Tukio hili linakuja siku chache tu baada ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga kuzuiwa kufanya kazi yao kwa kile kilichodaiwa kuwa hawapo kwenye msafara wa Magufuli....

SOMA HABARI YA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA KUINGILIWA UHURU WAO MKUTANO WA MAGUFULI HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527