Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Duh!! JAMAA KAKOSEA KUTUMA UJUMBE WA MANENO UKAENDA KWA POLISI ILI APATIWE DAWA ZA KULEVYA...KILICHOFUATA NI STORI




William Lamberson raia wa Florida,Marekani amejikuta mikononi mwa polisi baada ya kutuma ujumbe wa maneno kwa Polisi akidhani ni rafiki yake.

Ujumbe huo ulilenga kutaka apatiwe dawa za kulevya kutoka kwa rafiki yake huyo ambaye walikuwa wakishirikiana katika biashara hiyo lakini alikosea na kujikuta ukienda kwa Brian Bergen ambaye ni kiongozi wa Polisi.

Polisi walianza kufanya uchunguzi wao na kugundua Lamberson anajihusisha na uuzaji wa dawa hizo hivyo baada ya uchunguzi aliwekwa ndani na kufunguliwa mashtaka ya kujihusiha na biashara hiyo haramu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com