BASI LA CITY BOY LAUA WATU WATATU SINGIDA, WANANCHI WAFUNGA BARABARA, POLISI WAPIGA MABOMU





Jeshi la polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi Wa kijiji cha Itukutu kata ya Ulemo waliofunga barabara mkoani Singida baada ya basi la kampuni ya City Boy kugonga watu watatu usiku huu majira ya saa mbili.

Kwa mujibu wa mwandishi mkuu wa mtandao huu Kadama Malunde ambaye yupo eneo la tukio amesema taarifa za awali zinasema miongoni mwa watu hao watatu waliogongwa wawili wamefariki dunia, ndipo wananchi walipojitokeza na kuziba barabara, huku majeruhi mwingine akikimbizwa hospitalini kwa matibabu zaidi

Basi hilo lilikuwa likitoka Dar Es Salaam kuelekea Kahama ambapo linadaiwa kuwa katika mwendo kasi na katika harakati za kumkwepa mzee mmoja barabarani ilishindikana likamgonga mtu mzee mmoja na kisha kuwagonga watu wengine wawili waliopoteza maisha papo hapo


Hali hiyo ilisababisha wananchi kufunga barabara kwa matawi ya miti,mawe na kurusha mawe kwa basi lililosababisha ajali ingawa dereva alifanikiwa kuliondoa eneo la tukio huku mengine yakizuiwa kuendelea na safari

Tukio hilo lilidumu kwa takriban dakika thelathini na ndipo jeshi la polisi lilipofika na kufanikiwa kuwatawanya wananchi hao


Hata hivyo mabasi hayo yameruhusiwa kuendelea na safari

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527