ANGALIA PICHA KUBWA ZAIDI KUTOKA KWA MAGUFULI LEO,ATINGA KIJIJINI KWAKE CHATO HADI KWENYE KABURI LA MWALIMU WAKE

Dk Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu, Cornel Pastory


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi kwa wananchi huku akishangiliwa aliposimama kusalimia katika Mji wa Nyakanazi, wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera leo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG



Wakazi wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wakati wa mkutano wa kampeni

Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba za Dk Magufuli wilayani Kakonko, Kigoma



Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi Mgombea ubunge jimbo la Kakonko, Christopher Chizza wakati wa mkutano wa kampeni wilayani Kakonko, Kigoma.

Vijana wakisikiliza kwa makini wakati huku wakiwa juu ya baiskeli wakati Dk Magufuli akijinadi wilayani Kakonko

Dk Magufuli akiwafariji ndugu wa aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu Cornel Pastory alipozuru kaburi la mwalimu huyo wilayani Biaharamulo

Dk Magufuli akiwafariji ndugu wa aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu, Cornel Pastrory alipkwenda kuzuru kaburi

Mwalimu Cornel Pastory enzi za uhai wake

Dk Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu, Cornel Pastory

Dk Magufuli akiomba alipozuru kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu Pastory wilayani Biharamulo, Kagera.

Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni mjini Biharamulo leo

Mgombea ubunge Jimbo la Muleba Kusini kupitia CCM, Profesa Anna Tibaijuka (kulia) akiwa miongoni mwa walioshiriki katika mkutano wa kampeni za CCM mjini Biharamulo

Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akifanya kampeni mjini Biharamulo

Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini ili wampigie kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 Biharamulo

Ni furaha iliyoje kwa wakazi wa Bi9aharamulo baada ya kumuona Dk Magufuli wakati wa kampeni mjini humo leo

Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Biharamulo, Oscar Mkassawakati wa kampeni hizo leo






Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Chato,Meedard Karemani katika Kata ya Igalula wilayani Chato ambaye ndiye mrithi wake katika nafasi hiyo






Ulinzi ukiwa umeimarishwa nyumbani kwa Dk Magufuli, mjini Chato







Sura zikionesha matarajio makubwa baada ya kumuona Dk Magufuli alipowasili katika Kata ya Igalula alipozungumza nao na kupata wasaa kuwaaga wananchi wa Jimbo la Chato baada ya kufanikiwa kupata nafasi ya kugombea urais wa T anzania.






Sehemu ya wananchi wa Chato wakimlaki Dk Magufuli

Ulinzi ukiwa umeimarishwa baada ya Dk Magufuli kuwasili nyumbani kwake Chato baada ya kufanya kampeni katika Wilaya ya Biaharamulo, Kagera.

Dk Magufuli akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Fatma Mwassa

Dk Magufuli akisalimiana na ndugu zake akiwemo mamake mzazi (katikati) alipowasili nyumbani kwao Chato baada ya safari ndefu ya kufanya kampeni katika mikoa 13 nchini.

Dk Magufuli akisalimiana na ndugu nyumbani kwake Chato




Wananchi waishio katika mikoa ya Kigoma na Kagera wameiomba serikali ya awamu ya tano itakayoingia madarakani kuimarisha miundo mbinu hasa ya reli kwa kuunganisha na nchi jirani pamoja na uwepo wa bandari bubu ili kusaidia kuinua pato la taifa pamoja na uchumi wa maeneo hayo ambayo yako nyuma kimaendeleo ukilinganisha na maeneo mengine ya nchi.




Wananchi hao wametoa wito huo katika mikutano ya kampeni ya kusaka urais kupitia chama cha mapinduzi CCM na kuongeza kuwa baadhi ya maeneo ya mikoa hiyo kumebainika kuwepo na kiasi kikubwa cha maliasili yakiwemo madini na hivyo uwepo wa bandari ya nchi kavu pamoja na miundombinu ya reli kutasaidia kuchochea kukuwa kwa biasahara na hivyo kuinua vipato vyao na kuondoakana na umasikini.


Dr Magufuli ambaye amekuwa mkoani Kigoma akinadi sera za chama chake cha CCM na kuomba ridhaa ya watanzania kumpa kura ili aweze kuwa rais wa awamu ya tano ameanza kampeni zake mkoani Kagera ambapo akizungumza na wananchi wa eneo la Biharamulo amewahakikishia kuwatumikia watanzania kwa uaminifu na uadilifu na kuahidi kufanya jitihada za kukuza pato la taifa ili serikali imudu kutoa huduma za kutosha na za uhakika kwa jamii ya watanzania.


Akiwa wilayani Biharamulo mgombea huyo wa urais kupitia CCM Dr John Pombe Magufuli amehani msiba wa aliyekuwa mwalimu wake mkuu wa shule ya msingi marehemu Corneli ambapo kumefanyika sala fupi kwa ajili ya kumuombea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post