Taarifa tulizozipata ni kwamba Jeshi la polisi jiji Mwanza limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa vyama vinavyounda Ukawa ili wasiandamane kwenda uwanja wa ndege wa Mwanza kumpokea mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, aliyepo katika ziara ya kusaka wadhamini.
Mabomu yamepigwa muda mfupi baada ya ndege inayosadikiwa kuwa ni ya Lowassa kutua uwanjan, hali iliyowafanya wananchi walipuke kwa furaha huku wakiimba nyimbo za Chadema.
Kadhia hiyo iliwafanya Polisi watumie nguvu ya ziada kuwatawanya wananchi hao waliokuwa wametanda barabarani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Charles mkumbo, amesema mabomu hayo yametumika ili kuwazuia wafuasi hao wasiweze kujazana uwanjani hapo na kusimamisha shughuli nyingine.