News Alert!! KUHUSU TAARIFA YA MAKAMU WA RAIS KUIPIGA CHINI CCM NA KUHAMIA CHADEMAOfisi ya Makamu wa Rais inasikitika kuwepo kwa taarifa ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi. 

Tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais hajapanga tukio lo lote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.

Chanzo-ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post