Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MTOTO ALIYEPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA AKUTWA KWENYE PANGO MKOANI MWANZA


Mtoto wa miaka mitatu, Zainabu Adam, ameokotwa katika pango lililopo Mabatini Mtaa wa Nyerere A uliopo jijini Mwanza, baada ya kupotea nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha.

Akizungumza na Mwandishi wetu, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Hassan Maulid, alisema mtoto huyo alikutwa kwenye korongo hilo baada ya baadhi ya wakazi wa eneo hilo kusikia sauti yake wakati akilia.

“Tulipeleka taarifa kituo cha polisi Mabatini kuhusiana na kelele hizo, tuliongozana hadi eneo la tukio na waokoaji walizama ndani na kumuokota mtoto huyo"

Alisema walimpeleka kituo cha polisi mkoa wa Mwanza na kupatiwa PF3 na kumpeleka hospitalini kufanyiwa uchunguzi wa afya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com