KUHUSU TAARIFA ZA KIFO CHA PADRE EMMANUEL SOMBI WA SHINYANGA,MAZISHI YATAFANYIKA KESHO BUGISI




Padri Emmanuel Sombi enzi za uhai wake



Waamini wa Parokia ya Ngokolo jimbo Katoliki la Shinyanga leo wametoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Padri Emmanuel Sombi aliyekuwa mmoja wa maparoko wasaidizi wa parokia ya Sayusayu.


Padre Sombi amefariki dunia Julai 31 mwaka huu katika hospitali ya Bugando Jijini mwanza.

Mwili wa Padri Sombi uliwasili jana katika Parokia ya Sayusayu katika Jimbo katoliki la Shinyanga kutoka katika hospitali ya rufaa ya Bugando ambapo waamini na watu wenye mapenzi mema,walipata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.

 Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Askofu wa Jimbo la Shinyanga mhashamu Liberatus Sangu, Padre Sombi amefariki dunia majira ya saa tisa usiku wa kuamkia juzi katika hospitali ya rufaa ya Bugando Jijini Mwanza ambako alipelekwa kwa matibabu baada ya kuugua ghafla.

 Mazishi ya Padri Sombi yatafanyika kesho Jumatatu Agosti 03,2015 majira ya saa nne asubuhi katika Parokia Ya Bugisi.
Mungu ailaze mahali Pema mbinguni roho ya marehemu Padre Sombi Amen !

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post