Utafiti_HIZI NDIZO MBINU TATU ZINAZOTUMIWA NA MBU KUTAMBUA MWILI WA BINADAMU NYAKATI ZA USIKU NA KUUSHAMBULIA



Utafiti mpya umebaini kwamba mbu hutafuta kitu cha kula kwa kutumia vigezo vitatu,harufu,macho na joto.

Utafiti huo unasema kuwa mbu anaweza kufahamu aliko mwanadamu kupitia hewa ya kaboni ambayo watu hupumua nje.



Inasemekana mbu hunusa hewa hii kiasi cha mita 50.

Wanasayansi wamesema kwamba walimfuatilia mbu mwenye njaa, ndani ya mtaro uliofunikiwa.

Kisha waligundua kwamba mbu hao walianza kunusa nusa hewa ya kaboni, na kutema mapovu yenye matone meusi yaliowekwa na watafiti hao sakafuni.

Imebainika kwamba wakati mbu yuko mita chache karibu na kile anacholenga, huvutiwa sana na joto.

Hii imebainisha kwamba hata hufuata joto hilo na kisha kumshambulia mwanadamu.

Huenda ukapata Malaria au ukaponea lakini utakua na vipele pale vya mbu anapokuuma.

Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post