BAADA YA MGOMBEA KUPIGWA,NYINGINE HII HAPA KUHUSU WAFUASI WA MGOMBEA UBUNGE WA CCM KUPIGWA CHUPA,WAKO HOI HOSPITALIWatu watatu wamelazwa katika hospitali teule ya Shirati wilayani Rorya baada ya kujeruhiwa vibaya katika ugomvi ambao unadaiwa kuhusishwa na kampeni za kisiasa za wagombea wa ubunge wa Chama Cha Mapindizi katika jimbo la Rorya mkoani Mara.

Mmoja wa majeruhi wa tukio hilo, amesema walishambuliwa na chupa huku wakitishiwa kukatwa mapanga muda mfupi baada ya kumalizika mkutano wa kampeni za CCM katika eneo hilo.

Hata hivyo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rorya Bw Samwel Kiboye, amekiri kupata taarifa hizo kuhusu wafuasi wa mmoja ya wagombea kununuliwa silaha za jadi kwa ajili ya kuwashambulia vijana wa wagombea wengine.


Amesema mbali na tukio hilo kufikishwa katika vyombo vya dola pia chama hicho kitachukua hatua kali kwa wahusika huku mmoja wagombea Mh Lameck Airo akitishia kujitoa kugombea ubunge endapo vitendo hivyo havitadhibitiwa.

Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post