Taarifa Kamili!! BASI LAGONGA TRENI YA MIZIGO ,WATU WANNE WAFARIKI,25 MAJERUHI

Watu 4 wamefariki dunia papo hapo na wengine 25 kujeruhiwa vibaya baada basi la abiria kampuni ya badcard likitokea Kilosa kwenda Morogoro kugonga Treni ya mizigo ikitokea Morogoro kwenda Dodoma katika eneo la kibaoni wilayani Kilosa mkoani Morogoro. 


Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ACP Mussa Marambo amefika katika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo.


 Amesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari kutokuwa mwangalifu wakati akivuka reli na nakuwataka madereva kuwa makini na kuzingatia sheria wanapo vuka katika makutano ya reli na barabara ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima zinazogharimu maisha ya watu.

Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kilosa Dk Denis Haule amekiri kupokea maiti 4 pamoja na majeruhi 25 ambapo kati yao watano hali zao ni mbaya na wamehamishiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.


 Katika hatua nyingine amelalamikia shirika la umeme Tanzania Tanesco kuweka umeme wa luku katika hospitali ambapo wakati wa tukio la ajali imesababisha kero kubwa na kushindwa kuwahudumia majeruhi kwa wakati na kulazimika kuchukua muda mrefu kutafuta jenereta.

Nao majeruhi na mashuhudi wa watukio hilo wameeleza jinsi tukio lilivyotokea ambapo wametupia lawama dereva wa treni kutopiga honi kwa tahadhari na kusababisha ajali ambayo imegharimu maisha ya watu kwa kusababisha vifo, na vilema vya kudumu kwa abiria wasiokuwa na hatia.

Katika tukio hilo waliofariki ni mwanamke mmoja, wanaume wawili pamoja mtoto mdogo na kati ya majeruhi 25 watano kati yao ni watoto wadogo na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post